MWENYEKITI mpya wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dionis Malinzi, anatarajiwa kuanza kampeni ya kutembelea ofisi za vyama na mashirikisho ya michezo ili kuona uhai wao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa BMT, Maulid Kitenge, alisema kuwa Malinzi ataambatana na viongozi mbalimbali wa baraza hilo, ambapo lengo kubwa ni kupambana na wababaishaji walio kwenye vyama hivyo.
Kitenge alisema mbali na kubaini matatizo hayo, pia ataangalia changamoto mbalimbali zinazovikabili vyama hivyo, ili waweze kupambana nazo kwa ajili ya kuleta maendeleo katika sekta ya michezo hapa nchini.
“Haiwezekani tuwe na vyama vya mifukoni visivyo na ofisi za kueleweka, kwa kweli hivi hatuwezi kuvivumilia, kwa sababu utakuwa ni ubabaishaji tu,” alisema Kitenge.
Alisema kuwa Malinzi kutembelea vyama hivyo ni moja kati ya ahadi zake za awali, alizozitoa mara tu alipoteuliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, ambapo vyama vitakavyobainika havipo kihalali vitashughulikiwa.
Tanzania Daima
0 comments