Monday, November 28, 2011
MSUNI ACHAPWA MOROGORO
Aboodmsuni aliwasili Morogoro siku ya alhamisi ya tarehe 24 november na jana november 27 alivaa magwanda ya wafanyakazi wa chuo cha kiislam Morogoro kuwakabili wanafunzi wa mwaka wa pili.
Aboodmsuni anayetambulika kwa jina la Msuni katika mitaa ya Bima, Kihonda na kipa anaedakia timu ya Eleven Boys 'Cosovo' pale anapokuwa mkoani Morogoro, alichezea timu ya wafanyakazi wa Chuo hicho badala ya baba ake Dr. Hamdun Sulayman ambaye hakuwemo hapo jana.
Aboodmsuni alicheza kama beki namba 3 na akiwa ajagusa uwanja kwa takribani miezi miwili alijitahidi kuwazibiti washambuliaji hatari ya mwaka wa pili ambao walipata goli la kuongoza katika dakika ya 15 kwa shuti kali lililo mshinda mlinda mlango Gaddafi ambaye alionyesha Uhai katika kipindi Cha kwanza.
Pasi ndefu iliyopigwa na beki ya wafanyakazi ilikuwa inakimbilia kutoka nnje na mashabiki pamoja na kipa wa mwaka wa pili wakiamini Abdallah hato ukuta ule mpira na akaukuta na kuuleta kati ambapo ulimkuta Kamugisha akiwa na goli ambapo alisawazisha. Mpaka mapumziko Staff 1-1 wanafunzi.
Kipindi cha pili kilianza kwa wanafunzi kulisakama lango la Staff na kufanikiwa kupata goli kwa shuti la Umbali ambalo lilimshinda mlinda mlango Gaddafi ambaye kipindi cha pili alicheza chini ya kiwango.
Aboodmsuni aliwasazishia Staff kwa mkwaju wa penati kufuatia mchezaji wa wanafunzi kuunawa mpira katika eneo la hatari. Na Aboodmsuni ambaye anarikodi ya kukosa penati.
Baada ya goli hilo la Aboodmsuni wanafunzi walicharuka na kupata mpira wa adhabu ndogo ambao ulipigwa moja kwa moja mpaka nyavuni. Na mpira kumalizika kwa Wanafunzi kuibuka na Ushindi wa goli 3 dhidi ya 2 za Staff 'wafanyakazi wa chuo'.




0 comments