MWANAMKE mkazi wa Kijiji cha Kwisarara wilayani Tarime mkoani Mara, Maria Magaigwa (45) na mwenzake mkazi wa Kijiji cha Nkongore, Maxmillian Chacha (35), wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya hiyo wakikabiliwa na mashitaka ya kupatikana na mashamba yenye zao haramu la bangi ekari nne.
Wakisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime, Odira
Amworo, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Usu Chamba alidai mtuhumiwa Magaigwa
alipatikana na shamba la zao hilo ekari tatu, Desemba 11, mwaka huu mchana baada ya raia wema kutoa taarifa kuwepo shamba hilo.
Polisi walifanya msako na kufika katika shamba hilo na kumkuta Magaigwa ambaye ni mmiliki
wake na kumkamata na kumfikisha kujibu mashitaka ya kulima zao haramu. Amekana mashitaka hayo.
Mtuhumiwa wa pili, Chacha ilidaiwa alipatikana na kilimo cha zao hilo Desemba 12, mwaka huu
baada ya msako unaoendelea katika Wilaya za Tarime na Rorya dhidi ya walimaji zao hilo haramu, wapika gongo, wezi wa mifugo na vibaka. Mtuhumiwa alikana mashitaka hayo.
Habari leo
0 comments