Monday, April 9, 2012
Taarifa kuhusu ajali ya ndege
Abiria 35 na wafanyakazi wanne wa ndege ya shirika la Ndege Tanzania (ATC) wamenusurika katika ajali ya ndege (pichani juu) iliyotokea asubuhi ya leo majira ya saa 4.15 katika uwanja wa ndege wa Kigoma.
Habari za awali zinasema, ndege hiyo aina ya Dash 8-300 iliyokuwa inatoka Kigoma kwenda Dar es salaam kupitia Tabora iliopata ajali baada ya kuteleza na kuangukia ubavu wa kulia katika tope jingi lililopo katika njia ya kurukia ya uwanja huo.
Abiria na wafanyakazi wote waliokuwamo waliweza kutoka katika ndege salama muda mchache baada ya jaribio lake la kupaa angani liliposhindikana.
Baadhi ya abiria waliohojiwa baada ya ajali wamewasifia sana rubani Emmanuel Mshana na msaidizi wake Mbwali Masesa kwa kujitahidi kuidhibiti kiuweledi ndege hiyo na kuokoa maisha ya watu.
Uchunguzi wa awali unaonesha bawa la kulia pamoja na injini ya propel ya upande huo vimeharibika vibaya.
Kwa picha zaidi na maelezo bofya hapa
No comments:
Post a Comment