Katika
zoezi la kukusanya na kuwasilisha maoni ya Waislamu juu ya Katiba Mpya
vipo vyombo viwili kwa ajili ya Waislamu, vyote vikiwa na azma moja,
kulinda na kutetea maslahi ya Uislamu na Waislamu nchini. Vyombo hivi
ni:
1. Jukwaa la Waislamu la Kuratibu Mabadiliko ya Katiba Tanzania (JUWAKATA)
2. Mtandao wa Misikiti Tanzania
JUWAKATA
imekwishatoa maelekezo muhimu kwa Waislamu katika kijitabu chenye
anuani “MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA TANZANIA”. Jukwaa limefanya
kazi kubwa ya kupita katika mikoa mingi nchini kutupa maelekezo muhimu
na mambo ambayo Waislamu hatuna budi kuyapigania yawepo katika Katiba
Mpya. Mtandao wa Waislamu wa Mawasiliano na Kupashana Habari umepata
nakala ya kijitabu hiki chenye kutoa maelekezo kwa Waislamu.
Mtandao
wa Misikiti Tanzania umetoa MUHTASARI WA HOJA NA MAONI JUU YA KATIBA
MPYA kama yalivyokusanywa na kuratibiwa kutoka katika semina shirikishi
za mtandao wa misikiti nchini. Semina hizi zimefanyika katika mikoa 17
Tanzania Bara na mkoa mmoja Zanzibar. Mtandao wa Waislamu wa Mawasiliano
na Kupashana Habari umepata nakala ya kabrasha lenye hoja na maoni
haya.
Waislamu
hatuna budi kuwasilisha maoni yetu kama KUNDI MASILAHI na sio kama
Watanzania, au watu wa wilaya, mkoa fulani au wa kundi la aina yoyote
katika jamii ambalo halijinasibishi moja kwa moja na Uislamu. Katika
kufikia lengo hili Mtandao umeambatanisha katika waraka huu MUHTASARI WA
HOJA NA MAONI YA WAISLAMU JUU YA KATIBA MPYA.
Nia
na madhumuni ya kiambatanisho hiki ni kutoa fursa kwa Waislamu katika
kila kona ya nchi yetu ya kutoa maoni haya kwenye Tume ya Taifa ya
Kukusanya Maoni moja kwa moja kupitia E-Mail Address ya Tume (Anuani ya
Tume ya Barua Pepe).
Unaweza kuchagua idadi yoyote ya hoja na maoni (kwa jozi ya pamoja) na kuyatuma kwenye Tume kwa anuani ifuatayo: Email : maoni@katiba.go.tz
Ili maoni yako yapate tafsiri ya kutumwa na Muislamu kwa ajili ya Uislamu huna budi kujitambulisha kwa:
· Jina lako
· Mawasiliano ya Simu (kama una simu)
· Msikiti Wako Unakoswalia (Muhimu Sana)
· Wilaya na Mkoa (Ulipo Msikitin wako)
No comments:
Post a Comment