Thursday, August 9, 2012

Namna ya kumsaidia mama mjamzito

NI KWA KUTUMIA BINZARI NYEMBAMBA
Nimekulizwa sana kuhusu hili jambo ambalo liliwahi kuzungumziwa kwenye leo tena.Ni njia ya kienyeji ya kumsaidia mama mjamzito kujifungua haraka.Inatokea mama anapatwa na uchungu lakini mtoto anakawia kutoka yaani anachelewa kujifungua.
Binzari nyembamba hutumika sana kwnye mapishi ya pilau,supu au mchuzi.

Hapa kinachofanyika ni kuchemsha maji kisha unatia binzari nyembamba ichemkie humo.Unachuja na kumpa mama anywe yale maji baada ya hapo inachukua muda mfupi tu kisha mama hujifungua.
Hii si kwa mujibu wangu bali mmoja wa wasikilizaji wa leo tena alitufahamisha.



Kutoka kwa: Dina Marious

No comments:

Post a Comment