Kutoka Facebook:
Waziri wa afya nchini ni miongoni mwa mawaziri muhimu sana katika ujenzi wa taifa, taifa lilojaa magonjwa ni taifa mfu.
Hivyo lazima wizara hii iongozwe na mtu makini na mchapakazi, mwenye malengo na uzalendo kwa nchi yake.
Hapa kwetu wizara hii kapewa ndugu yangu Hussein Mwinyi sio siri wala siogopi kazi kashindwa na wizara haiwezi, tokea muda alioteuliwa mpaka sasa hajatuambia watanzania yeye na wizara yake mipango mizuri ya kutupa afya bora, mpka leo wizara yako imeshindwa kupunguza au kupambana na magonjwa mfano TB ambayo kwa muda yalipungua nchini, Mwnyi kashindwa kutetea mpango wa malaria ambao unaendelea kutumaliza kila siku na ukweli umefeli, hali ya vituo vya afya ki usafi na mazingira inazidi kudorora wakati taifa linaingia katika teknologia wizara afya inazidi kurudi nyuma.
Mengi nikiandika hapa hayatoshi ila kwa mtu mwenye akili anaona. Mwinyi pumzika au zinduka sasa ndugu zako tunakufa na maradhi
No comments:
Post a Comment