Saturday, October 6, 2012

LALA NA HII, TURUDI MWANZO


Na Rajabu Omary, Facebook:

Jamaa watatu walikodi hotel yenye gorofa 60, wao wakapata gorofa ya mwisho kabisa.

Wakapanda kwa lifti na asubuhi wakashuka kwa lifti. Jioni waliporudi wakakuta umeme umekatika.

Wakakubaliana wapande ngazi kwa story. Wa kwanza apige story za kutisha kuanzia gorofa ya 1 mpaka ya 20, wapili apige strory za kuchekesha kuanzia gorofa ya 21-40 na watatu mwanawane akandamize story za kuhuzunisha kuanzia gorofa ya 41-60.

Walipofika ya 59 yule watatu akasema hii ndio ya kuhuzunisha zaidi...TUMESAHAU KUCHUKUA FUNGUO PALE RECEPTION.

No comments:

Post a Comment