Thursday, February 21, 2013

MIAKA MIWILI KATIKA TASNIA YA BLOG KWA MSUNI

Blogger na computer technician wa ABOODMSUNI NETWORK, Abdallah Hamdun Ibrahim Sulayman 'Msuni' leo usiku anataraji kutimiza miaka miwili toka aanza taratibu za kuendesha blog na shughuli za ABOODMSUNI NETWORK kuanza rasmi

Ilikuwa ni jumatatu ya tarehe kama ya leo (21/02) mwaka 2011, mida ya saa moja kasoro (7:45) usiku akitokea kwenye darasa la kusoma kiarabu nchini Sudan katika jiji la Khartoum Msuni kwa mara ya kwanza alijitambulisha katika blogger baada ya kuiachia blog ya SPORTS IN BONGO.

SPORTS IN BONGO (SIB) ndio blog ya kwanza kuanza kazi katika blogs zinazosimamiwa na ABOODMSUNI BLOGS ikifuatiwa na blog ya ABOODMSUNI NETWORK iliyofunguliwa wiki 2 baada ya SIB kuanza kazi ikiwa na malengo ya kuripoti shughuli za mmiliki wa ABOODMSUNI NETWORK na shughuli zinazo fanywa na ABOODMSUNI NETWORK.

Kuanza kwa SIB iliyokuwa inajulikana kwa jina la TANZANIA FOOTBALL EVENT ilikuwa ndio mwanzo wa shughuli za ABOODMSUN NETWORK zikianzia katika uendeshaji wa blog ya SIB na namna ya kusimamia blog xako.

Msuni mtoto wa 4 wa muhadhiri wa chuo cha waislamu Morogoro (MUM) Dr Hamdun Ibrahim Sulayman ndiye mmiliki halali wa ABOODMSUNI NETWORK inayojihusisha na shughuli za kutengeneza blog, website na ukarabati wa computer.
--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

No comments:

Post a Comment