Tuesday, February 26, 2013

MSIBA KWA WAISLAM: IMAN FM YAZIMWA

Iman fm imezimwa hivi punde katika kutii amri ya chombo kilichopewa dhamana ya kusimamia vyombo vya habari hapa nchini TCRA.

TCRA leo mchana saa sita ilitangaza kuifungia iman fm inayomilikiwa na islamic foundation yenye 6ffici yao Morogoro mjini miezi 6 pamoja na onyo kali kwa madai ya kuhusishwa katika kuchochea waislam kugomea kuhesabiwa katika wakati wa sensa.

Akizungumza na wasikilizaji wa iman fm saa moja na nusu usiku huu mwenyekiti wa islamic foundation Khalif Nandi amesema kuwa wanatii amri ya TCRA kwa kuzima mitambo ya imani fm mara baada ya kumalizika kwa maongezi yake.

Nandi amewataka waislam wote na wasikilizaji wa imani fc kuwa na subqa katika kipindi chote hicho, na hii ni miongoni mwa qadari.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION TUPO PEMBA FEB 21-MACH 15
TUNAREKEBISHA COMPUTER ZILIZO KUFA
Wasiliana na HABIB KHAMIS: +255-657-148-283
www.aboodmsuni21.blogspot.com

No comments:

Post a Comment