Saturday, September 20, 2014

SIB DAKIKA 90 IMEREJEA KIVINGINE

Ikiwa leo pazi la ligi kuu ya vodacoma ina funguliwa rasmi kwa michezo 6 katika viwanja 6, Aboodmsuni Network inataraji kurejesha huduma ya livescore ya soka la bongo kupitia ukurasa mpya wa SIB DAKIKA 90.

Ikimbukwe kuwa Aboodmsuni Network kupitia blog zake za Chama lamgu Ni Azam na Sports In Bongo ilikuwa inaleta livescore ya soka la bongo kabla ya kuingia kwa mwaka huu, ambapo ilisitisha shughuli hiyo katika blog zake.

Tunekuwa tukipokea messeji za wadau mbalimbali kuhusu uhitaji wa kurejeshwa kwa kipengele hicho katika blog zetu ambapo jumapili iliyopita (september 15) tulirejesha huduma hii katika ukurasa wetu mpya wa SIB DAKIKA 90.

Ukurasa huu mpya utamuwezesha mdau kufuatilia pia livescore za ligi mbalimbali ulimwenguni, sambamba na ratiba, matokeo na msimamo wa ligi.

Katika kuhakikisha tunatatua kiu ya wapenzi wa Blog za Msuni tutakuwa na unaifanya maboresho kadri ya uwezo wetu na kukata kiu ya wadau wetu.

Ukurasa wetu huo ambao link zake zimeanza kuonekana katika blog zetu mbalimbali sambamba na kwenye facebook account zetu ina kwenda kwa link ya www.amsuni.host56.com.


Imetolewa na: Abdallah H.I Sulayman
msimamzi wa Blog za Msuni

No comments:

Post a Comment