Friday, August 5, 2011

Kwanini twafunga

Mwezi wa Ramadhani umeingia majuzi na baadhi ya watu wanaacha chakula na vinywaji vyao mchana kutwa katika mwezi mzima wa Ramadhani wakisema wamefunga. Je kwa nini watu waache chakula chao siku 29 zote?

Jawabu la swali hili linapatikana kwenye Kitabu wanacho kifuata Qur an ambapo inasema wamefadhilishwa kufunga ili wawe wachamungu. "Enyi mlioamini mmefaridhishwa funga kama walivyofaradhishiwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu." (2:183)

Kama kujizuia kula mchana kunampelekea mtu kumuhofia Mungu muumba (kumcha Mungu), ni vipi kujizuia kula kunamjenga mwenye kufanya hivyo kumuhofia Mungu Muumba.

Jawabu linapatikana ndani ya maana ya funga. Kwani funga si kuacha kula na kunywa kama wengi wanavyo fanya bali kunamambo mengine ambayo yanamfanya mtu aliyejizuilia kula kujihesabu kafunga.

Maana ya Funga kisheria ni kujizuilia kula, kunywa na kujiepusha kutazama wanawake kwa matamania na yenye kufunguza tangu kuchomoza kwa alfajiri mpaka kuchwa kwa jua. Yenye kufunguza funga yako mengi ambayo mengine ni halali kama ujafunga na ukifunga huruhusiwa kuyafanya kama kufanya tendo la ndoa na mkewe.

Na kuna yale ambayo moja kwa moja ni hayaruhusiwi kuyafanya wakati wote wa maisha yako kama kusengenya, kusema uongo na kadhalika. Yote hayo ukijizuilia nayo kwa kuwa na hofu ya kuto haribu funga yako, ushinda njaa kwa faida kunakupelekea katika kumuogopa Mungu muumba na hivyo kufuata maamrisho yake na mwisho wa siku unajikuta ni miongoni mwa waja mnao mcha Mungu.

Tukiacha katika makatazo vilevile amali za mtu mwenye kufunga zimepandishwa daraja na hivyo kumfanya mwenye kufunga kuzidisha katika matendo hayo. Hivyo kumjenga mja katika misingi ya ibada ambapo kuna mplekea kuwa mchamungu.

Hivyo mwenye kufunga ipasavyo mwisho wa siku anajikuta yumo miongoni mwa waja wanao shikamana na maneno ya Mungu Muumba.

0 comments