Wednesday, August 3, 2011

Mwezi wa toba

Tuko katika mwezi wa Ramadhani, mwezi ambao Qur an iliteremshwa kwenye arshi ya dunia kabla haija teremka kidogo kidogo kwa Mtume Muhammad (s.a.w).

Mwezi huu wa Ramadhani unatambulika kama mwezi wa toba kwa kuwa mpaka mwisho wa mfungo wa Ramadhani muumini aliyejiepusha na matendo yote ambayo Allah (s.w) ameyakatiza atakuwa huru na moto wa Allah (s.w). Ndani ya mwezi huu wa Ramadhani kunapatikana kumi la maghfira (toba) ambapo waumini wasamehewa madhambi yao.

Hakiki sisi wanaadamu ni wakoseaji na mbora wetu ni yule anayetambua alipo kosea na kurejea kwa Allah (s.w) na kuomba msamaha huku aki kili kutorejea tena katika kosa hilo alilofanya.

Kama Muislam mwenye kufunga mwezi huu wa Ramadhani hauna budi kuomba msamaha kwa Allah (s.w) huku tukijizatiti kwenye njia yake ndani na baada ya mfungo huu wa Ramadhani.

Ni wakati vile vile wa kusameheana, kumaliza tofauti tulizo nazo. Ramadhani ikiisha ituache kwenye umoja ambao tunafuata Qur an na Sunna za mtume Muhammad (s.a.w).

0 comments