Wednesday, August 10, 2011

Mafuta+Umeme+Maji=foleni

Tanzania, Tanzania nchi ya wazee wangu niliyokulia na mwisho wa siku kuwa mmoja waraia watanzania. Tumepita kwenye vipindi vingi vya porojo, kusema saana utendaji unakadiriwa kufika asilimia moja ya tunavyo sema.

Tulimkaribisha Kikwete ikulu mwaka 2005 kwa sera yake ya ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya. Ila mwaka uliofuatia tukaingia kwenye mgao wa umeme huku Maji yakiendelea kuwa tatizo kwa maeneo mbalimbali ya Dar es salaam huku asilimia kubwa ya watanzania wakiwa hawajafikiwa na huduma hiyo.

Mgao wa umeme ukatuingiza katika mikataba mibovu na makapuni hewa kama hiyo haitoshi likaibuka Deci. Tumezoea kupanga foleni kwenye mahospitali, kunye vituo vya kuteka maji na kwenye kununua Luku. Likaja hili la foleni kwenye barabarani, huku kwenye daladala mwenye ubavu ndiye anae panda.

Tukamrejesha tena ikulu japo wapo wanao sema kura lizichakachuliwa akiwa na sera ya nguvu zaidi, kasi zaidi na ari zaidi. Hata mwaka ajachukua Tanzania imeingia kwenye giza tena la mgao wa umeme ambao haijulikani utaisha lini.

Huku akijikuna kichwa na kutafakali namna ya kuondoa adha ya umeme ambayo imewanufaisha waagizaji wa magenerater , likaibuka mabomu ya Gongolamboto, huku suala la katiba likiichefua serikali yake.

Tumetoka kwenye foleni ya maji na barabarani ambapo bado zinaendelea, tumeingia kwenye mafuta ambapo ilikuwa ndoto kutokea, lakini sasa yametokea.

Mafuta imekuwa bidhaa adimu, sikwamba hayapo wala watumiaji wameongezeka bali wahagizaji wameyazuia kuingia kwenye soko kwa kutaka serikali watimeze matakwa yao.

Serikali wametishia kuwafutia leseni lakini waheshimiwa hao wameendeleza na msimamo wao, ambao unahatarisha mambo mengi. Ni sheli chache zinazotoa huduma hiyo ya mafuta ambapo inakadiriwa kama hamna.

Hii ndio Tanzania ambayo inaongozwa kwa porojo na leo idadi ya magari imepungua barabarani.

0 comments