Wednesday, August 10, 2011

Utabiri wa usafiri jijini Dar es salaam hii leo

Nikiwa njiani asubuhi hii nikielekea college maeneo ya Tangbovu, Mbezi beach. Kama kawaida yangu ya kukata moja moja toka maskani Mikocheni kupitia barabara ya Kawe kama sikosei inatambulika kwa jina la Old Bagamoyo road nimekutana na hali tata.

Kama bado ujatoka nyumbani beba nauli ya ziada kwani kuna kila dalili ya nauli kupanda maradufu, kutokana na hadha hii ya mafuta, na ukiona Daladala usiseme limejaa sana lasivyo utajikuta utoki kituoni.

Mwendo wa dakika 15 mpaka 20 nilikuwa kwenye barabara ya kawe kuanzia kituo cha njiapanda ya Coca mpaka kwenye round about ya njia ya kuelekea Mbezi beach nimepisha na daladala 6 huku zikiwa zimejaza kupita maelezo.

Magari barabarani yamepungua kwa kiasi kikubwa, ile foleni niliyo zoea kuiona haipo leo. Hakikisha gari lako linamafuta ya kutosha na punguza mizunguko.

Kwa hali inavyoonyesha watumizi wa dalala waandae misuli yao kwa kugombania daladala kwaleo ni tofauti kabisa na siku nyinginezo.

Angalizo toka kwenye mitoko muhimu hata ukikosa usafiri waku kurudisha huto juta kutembea.

0 comments