Tamasha la eid fitri lililoandaliwa na taasisi ya Islamic Foundation inayomiliki redio iman ya Morogoro, inayoenda nakauli mbio la Tabasamu hii Ni sunna imefanyika kwa mafanikio ndani ya uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Tamasha hilo lililo anza saa 6 mchana lilifika tamati saa 2 usiku hii leo, wakati Aboodmsuni alitoka uwanjani hapo saa 12 na dakika 45 mara baada ya swala ya magharibi iliyoswaliwa kwa mara ya kwanza katika historia ya uwanja huo hii leo.
Maudhurio yalikuwa makubwa toka kwa wakazi wa Morogoro pamoja na vitongoji vyake, ambapo michezo ya beiskili, kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, kucheza mpira, kuvuta kamba, kula maandazi na maonyesho toka kwa vijana waskauti vilitendeka kwenye tamasha hilo lililo rushwa moja kwa moja na redio Iman FM.
Mchezo wa kukimbiza kuku ulivutia wengi ambapo ulifanywa kwa awamu nne, ukifuatiwa na maonyesho toka kwa vijana waskaut wakinogesha tamasha hilo.
Mbio za Beiskili zilizo anzia katika msikiti wa Haki uliopo Morogoro nao ulikuwa na msisimko wake baada ya washindanaji wakipishana kwa nafasi kubwa. Mshindi wa kwanza aliwaacha wenzake mbali kiasi kwamba iligharimu dakika 8 mpaka mshindi wa pili alipo wasili hapo Jamuhuru, huku kukimshuhudia mzee mmoja akishika nafasi ya 6 na kutunukiwa zawadi kwa kuweza kumaliza mashindano na kuwa ni mtu aliyekula chumvi nyingi kushiriki mbio hizo.
Mbio za beiskeli za miguu mitatu ilifanyika hapo na washindi kupata zawadi na huku washiriki nao wakipewa kifuta jasho. Kiburudisho kingine kilikuwa kwenye mbio za magunia ambapo kulishuhudia baadhi ya washindani wakishindwa kukamilisha shindano.
Mbio hizo za magunia yalikuwa niya mita 100 kwenda na kurudi na hivyo kufanya ziwe mita 200 huku kijana toka kwenye timu ya skauti akiibuka kinara. Swala zote ziliswaliwa hapo viwanjani kuanzia adhuhuri mpaka Magharibi huku waumini na wasikilizaji wa Iman FM walipata fursa ya kuwaona watangazaji na waanda vipindi vya Iman FM.
Mida ya saa 11 mchezo wa soka ulichukua nafasi ukishuhudia kombain ya Morogoro iliyokuwa inaundwa na wafanyakazi wa Iman FM pamoja na wafanyakazi toka sehemu nyingine wakimenyana na Kombaini ya Kibaha ambapo Morogoro waliibuka kidedea.
Kombaini ya Morogoro ilicheza na wafanyakazi wa chuo cha kiislamu Morogoro (MUM) na mchezo kukamilika kwa sare na kushuhudia Aboodmsuni akicheza timu na babaake Dr. Hamdun Ibrahim Sulayman ambaye ndie aliye funga goli la kuongoza kwa timu MUM kwa mpira wa adhabu ndogo uliotinga moja kwa moja nyavuni, kabla Moro kusawazisha goli hilo katika kipindi cha pili cha mchezo.

0 comments