Friday, August 12, 2011

Tuwe makini kwenye upangaji wa swafu tukielekea kwenye swala

Assalaam Alykum Warahmatullah Wabarakat.
Namshukuru Allah (s.w) kwa kuniwezesha kufika ijumaa ya pili ya mfungo wa Ramadhani huku ikiwa ni siku ya pili katika kumi la pili la Ramadhan.

Allah (s.w) ametoa kemeo kali kwa wale wanao swali, kwa kuzipuzia swala zao katika Qur an tukufu. Swala ndilo jambo la mwanzo kuulizwa mbele ya Allah (s.w) katika siku ya malipo.

Swala mpaka kukamilika kwake kuna vipengele vingi ambavyo mwenye kusimamisha swala anatakiwa kuvifuatwa. Hapa nataka kuzungumzi kipengele kidogo sana katika swala za jamaa, na labda inaweza ikawa ni moja ya sababu tusifikie lengo la swala, ambalo ni kumuepusha mwenye kuswali na mambo maovu na machafu.

Ili swala ya jamaa ikamilike inahitaji upangwaji safu za maamuma (wanao kuwa nyuma ya imamu). Na namna ya kupanga swafu mtume Muhammad (s.a.w) ametuelekeza.

Kwa kipindi cha hivi karibuni nimekutana na upangaji wa swafu tofauti na ule unao fafanuliwa na vitabu vingi vya swala. Nimekutana na upangaji wa Swafu wa kuanzia pembeni na kuanzisha swafu mpya kabla ya mwanzo kujaa na vile vile kujaza upande mmoja.

Kwa vitabu nilivyo pitia sijakutana na utaratibu huo nilio utaja hapo juu. Swafu hupangwa kuanzia katikati ambapo mara nyingi huwa ni mgongoni mwa imamu, na ujazaji wake unaanzia upande wa kulia kwa staili ya kusawazisha (upande wa kulia usimzidi upande wa kushoto).

Swafu ya pili haijazwi mpaka swafu ya kwanza ijae. Na ile misikiti ambayo imeongezwa pembeni bila ya uzio (ukuta) wa mwanzo kuondolewa, unatakiwa kujazwa katika eneo la mwanzo kwa mtindo ambao nimeueleza hapo juu, na kisha kumalizia katika eneo lililo ongezwa kwa kuanzia pembeni kwa upande ambao unaambatana na eneo la awali.

Tunatakiwa kuwa makini katika swala zetu kwa kufuata masharti na nguzo za swala ili tuwe wenye kusimamisha swala na wala tusiwe wale walio kemewa ndani ya Qur an.

Ijumaa karim

0 comments