Waislamu kote ulimwenguni hii leo wanasheherekea siku ya Edil Fitri baada ya kukamilisha swaum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ulifikia tamati hapo jana.
Japo kuwa Tanzania sio siku inayotambulika kama siku ye eidil Fitri kutokana na watu waliopewa dhamana ya kutangaza mwezi kukanusha taarifa za mwezi ulio shuhudiwa katika maeneo ya Mtwara na jirani zetu Uganda na mahali penginepo Duniani, lakini idadi kubwa ya waumini wa Kiislamu walijitokeza katika viwanja mbalimbali vilivyo swaliwa swala ya Eidil Fitri.
Katika viwanja vya Islamic Foundation vinavyo angaliana na hoteli ya Hilux jijini Morogoro kulikuwa na idadi kubwa ya waumini ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Katika viwanja hivyo vya Islamic Foundation, swala ya eid iliswaliwa saa mbili na robo asubuhi na kufuatiwa na hotuba ambayo ilikuwa ina wakumbusha waislam kutokimbia misikiti baada ya Ramadhani kwisha.
Muhutubiaji alisema kuondoka kwa Ramadhani isiwe sababu ya kurudi kwenye maovu waliyo yaacha kwa mwezi mzima. Vilevile alikumbushia suala la kuvikisha elimu ya kumtambua Allah (s.w) ndani ya Familia zetu.












0 comments