Wednesday, August 24, 2011

Zakatul Fitri

Assalama alaykum warahmatullah wabarakatu.
Namshuku Allah (s.w) kwa kunipa afya ya kuweza kufika siku ya leo ya Ramadhani ya 24 ikiwa ni sawa na agust 24.

Tukiwa tunaelekea mwisho wa Ramadhani basi maandaliza ya idil fitr ndipo yanapoanza. Waislam wanapanga namna ya kusheherekea kuhitimishwa kwa mafunzo yaliyo kuwa yanapatikana ndani mfungo wa Ramadhani.

Moja ya maandalizi muhimu ya idil fitri ni kuanda zakatul fitri ambayo hutolewa kabla ya swala ya eid. Napenda kuwakumbusha ndugu zangu waislam tukiwa tunautafuta usiku wa laylatul kadri tuwe tunaanda zakatil fitri ambayo huanzwa kukusanywa siku tatu za mwisho za mwezi huu wa Ramadhani mpaka kabla ya swala ya eidil fitri.

Zakatul fitri ndio msindikizaji wa funga zetu, hivyo kwa wale wanao wajibika kutoa hawana budi kuitoa.

Nikigeukia upande wa pili napenda kuwataadhirisha ndugu zangu waislam ambao wamepanga au wanapanga kusheherekea siku ya eidil fitri kwa kumuasi Allah (s.w) wavunje mipango yao hiyo kwa kuwa Allah (s.w) anasema atakae fanya maasi siku hiyo ye eid ni sawa na kufanya maasi kwenye uwanja wa hukumu hapo siku ya kiama.

0 comments