Nikiwa katika pilika pilika zangu Morogoro jana alasiri nusura daladala linikumbe mie na mwenzangu wa mbele kufuatia kuover take kwa upande wa kushoto.
Daladala mbili zilikuwa zinafukuzana katika barabara ya kuelekea Dodoma katikati nwa vituo vya Islam na Magorofani, ambapo aliyekuwa nyuma akaingia upande wa kushoto kutaka kumpita mwenzake wakati mbele yake nikiwa mie nikiendesha beiskeli ambapo alinipita kwa kasi, kitendo ambacho ilikuwa kidogo nivae body la gari huku jamaa aliyekuwa mbele yangu akiwa kampakiza mtu kwenye baiskeli ama nusura atoke kwenye barabara na kuingia bondeni.
Jamani twakuombeni tena kwa mara nyingine baada ya ile ya november 3 mwaka huu, ambapo nilizungumzia hili suala la kutanua upande wa kushoto, ambapo kwa jijini Dar es salaam hufanywa kutokana na foleni, ila unahatarisha Usalama kwa waenda kwa miguu.
Haraka zenu isi sababu ya kutuweka ulemavu watumiaji wa barabara wengine.
Tuesday, December 27, 2011
Related Post
0 comments