Hali ya mafuriko jijini Dar es salaam, huenda ikatokea tena kufuatia taarifa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa, hivyo kuwataka wananchi waliokuwa mabondeni kutoka.
Taarifa nilizo zipata alaasiri hii, inasemekana mto Msimbazi umeanza kutapika kufuatia mvua zilizonywesha jana usiku katika baadhi ya maeneo.
Director general wa mamlaka ya hali ya hewa Dr Agness Kijazi, amesema kuwa mvua kubwa zinatarajiwa kuanza kunyesha kuanzia leo hii.
Mamlaka za jiji la Dar-es-salaam, jana walireport kuwa mpaka sasa ni watu 40 waliopeteza maisha na zaidi ya watu 5,000 wamebaki na bila makazi kutokana na mvua za siku tatu mfululizo kusababisha mafuriko baadhi ya maeneo jijini Dar-es-salaam, ambayo mamlaka ya hali ya hewa wameelezea kama ni mvua kubwa kunyesha kwa kipindi cha miaka 57 iliyopita.
Tuesday, December 27, 2011
Related Post
0 comments