Saturday, December 17, 2011

Tujitokeze Taifa, kuichangia TV IMAAN


Shughuli nzima kesho iko Taifa kuanzia saa mbili asubuhi mpaka kumi na mbili jioni katika kongamano la kuchangi TV IMAAN, ambapo kutakuwa na mashekhe mbalimbali watakao pewa fursa ya kufikisha ujumbe kwa waislamu watakao hudhuria katika kongamano hilo.

Ni kongamano la kwanza la kuchangi TV IMAAN ili iweze kuruka hewani hivi punde, na kuwa TV station ya kwanza ya kiislam Tanzania, jambo ambalo tulikuwa tuna lipigia kelele.

Ni wakati wako wa kukizana na Shetani na kufika katika kongamano la kuchangi TV IMAAN ili tufanikishe ndoto yetu ya kuwa na kituo cha luninga cha waislam.

Jitokeze katika kiwanja cha Taifa ukiwa na swadaka yako ya kuchangi TV IMAAN kama utashindwa fika Taifa kesho kwa nyuzuru kama ilivyo kwangu, mchango wako unaweza kuutuma kwa njia mbalimbali ikiwemo M-PESA, Z-PESA ama kuweka katika Benki kama ilivyoelezwa na ndugu ARIF kupitia Radio Imaan na katika facebook (TIF).

Toa kwa mkono wa kulia wa kushoto usijue ulichotoa na kwa hakika taraji malipo toka kwa Allah (s.w).

TUKAUJAZE UWANJA WA TAIFA HAPO KESHO

0 comments