Leo katika uwanja wa Taifa kuna kongamano la kuchangia TV IMAAN ambapo limehudhuriwa na waislamu lukuki toka kona mbalimbali za Tanzania, huku mashekh wakinogesha kongamano hilo ambalo kauli mbiu yake Tumeahidi, Tunatimiza na Allaah shahidi.
Mgeni rasmi wa kongamano hilo alikuwa makamu wa pili wa Raisi Zanzibar, Maalim Seif Ahmad Shariff ambaye alihutubia ummah wa kiislamu, na ameongea mengi huku akigusia uonevu unaofanyiwa ummah wa kiislamu, huku Umati wa kiislamu ulio hudhuria kongamano hilo wakipiga Takbiri kila atoapo maneno.
Mashekhe mbalimbali walipata nafasi ya kuzungumza akiwemo Sheikh Nurdeen Kishkiy ambaye alisema, "Islamic foundation, wametuwezesha kuinua vichwa vyetu, kuinua macho yetu, kuinua mabega yetu, sasa tunaweza kutembea kifua mbele."
Na sheikh Twaabane, alikuwa miongoni mwa masheikh waliopata wasaa wakuzungumza ambapo alizungumzia mada ya Umuhimu na Upashanaji wa Habari Katika misingi ya Kitabu na sunnah.
Shekh Ally Baswalehe ndiye aliyefunga ukurasa wa nasaha za mashekhe ambapo alihitimisha kwa kugusa maeneo yaliyozungumzwa na mashekh waliyopata nafasi ya kuzungumza kabla yake, huku akitoa utafiti wa mwanamtafiti mmoja wa kizungu ambapo aliorodhesha watu 100 wa ajabu, ambapo Mtume Muhammad (s.a.w) ndiye anayefunguwa listi hiyo.
Kutokana na wingi wa mashekh ilibidi waendeshe tanbihi ya nani aongoze swala ya Adhuhuri ambapo ilimuangukia Shekhe Jabir Katura.
0 comments