Thursday, January 12, 2012

Wazazi kuchangia gharama za mitihani

Halima Mlacha

Serikali imesema, wazazi na walezi watalazimika kuchangia gharama za mtihani wa kidato cha pili, cha nne na cha sita, kutokana na gharama halisi kuwa mzigo mkubwa kwa Serikali.

Naibu Waziri alisema Serikali imekuwa ikigharamia mtihani wa kidato cha pili tangu mwaka 1984 ulipoanza rasmi hadi mwaka 1994 ulipositishwa na kurejeshwa mwaka 1999 wazazi walipoanza kuchangia gharama za uendeshaji wake kwa Sh 10,000 hadi Serikali ilipositisha hatua hiyo.

Alisema kwa sasa, uendeshaji wa mtihani huo umekuwa aghali kutokana na ongezeko la gharama sambamba na ongezeko la idadi ya shule na wanafunzi ambapo katika miaka ya 90, shule zilikuwa takribani 1,000 lakini sasa ni 4,367 hali inayofanya gharama kuwa kubwa.

“Hivyo Serikali imeamua katika mtihani huu wa kidato cha nne wazazi watachangia Sh 10,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule zote za Serikali na binafsi, pia wazazi watapaswa kuchangia gharama za uendeshaji wa mitihani ya Taifa ya kidato cha nne na sita kwa Sh 5,500,” alisema.

Alisema katika mitihani ya mwaka jana pekee, Serikali ilichangia zaidi ya Sh bilioni 28 na gharama ya mwanafunzi mmoja katika mitihani hiyo ni Sh 62,000.

0 comments