Sunday, May 8, 2011

Siwezi Kumlipa

aamsuni:

salamu natoa, maamukizi yaliyo makini,
namshukuru mola, aliyenipa pumzi hii,
mali akampatia, kunikopesha mimi,

pumzi yake nimeitumia, hata chakula pia,
nikamzoofisha kiafya, uchungu nikampatia,
hakanileta kwenye dunia, upendo akajazwa,

aliweza kunitupa, chooni ni kapotea,
sikuwa na ujanja, hata wa kukaa,
nilipolala nimelala, haja apo apo ninafanya,

kinyesi akagusa, kuniweka msafi daima,
wasiwasi humpata, asikiapo nikilia,
mengi amenifanyia, siwezi kuyamaliza,

nimekuwa mikononi mwake, kujifunza kuongea,
kanifundisha mengi, mwalimu bora sijawahi pata,
bado namwendea, kila nikitatizika,

ninadeni kubwa, ukubwa wa maisha,
nimeangaika kulipa, hata robo siwezi fika,
litanigarimu maisha, hata nusu ya robo sijafika,

kumlipa lazima, haitaji mali wala pesa,
wema kumtendea, dua kumuombea,
siwezi kumkimbia, kutoroka pia,
hakika nimekopa, siwezi kumlipa.



aboodmsuni sites like to say HAPPY MOTHERS DAY YOUR MY MIRROR IN MY LIFE, ONE LOVE TO ALL MOTHERS.

0 comments