Wednesday, June 1, 2011

Njoo tuzungumze


Wanafunzi wa shule ya sekondari Tosamaganga ya mkoani Iringa walijikuta katika hali ngumu baada ya kupigiwa mabomu ya machozi katika maandamano yao hapo majuzi.

Hili tukio na matukio mengine yanayo endelea maeneo tofauti nchini inaleta taswira mbaya katika nchi ambayo inajigamba ni nchi ya amani. Matukio haya ya kupigwa mabomu ya machozi katika hali ya watu kutoa kinunguniko chao kwa wenye madaraka kwa njia ya amani bila gasia, inaonyesha namna gani uhuru wa kujieleza unavyo pindishwa nchini.

Hao ni wanafunzi ambao ni viongozi wa kesho wa taifa, mnaanza kuwapiga mabomu pale walipotaka kutoa kero yao, unatarajia kitu gani toka kwao hapo baadae kama sio kutawala kiubabe kama anapitia huku ambako hatakiwi kusikilizwa kero yake, atasikiliza kero ya mtu kweli.

Watanzania tumekuwa walalamikaji sana pale tunapo ona tunadhulumiwa, ila dhulma ikizidi watavua magamba na kufanya kwa vitendo ambako kutaondoa hiki kineno cha kisiwa cha amani na kuwa kisiwa cha ghasia.

Tafadhalini wenye madaraka tumieni nyazifa zenu vizuri, kwa kutopindashi haki za binadamu. Kitendo cha kuwapiga mabomu ya machozi waandamaji si ungwana.

aamsuni

0 comments