Friday, September 23, 2011

Hotuba ya ijumaa; mambo manne muhimu kwa muislam

Assalam Alaykum warahmatullah wabarakatuh.

Namshukuru Mola kwa kunifanya nifike wakati huu, nikiwa na afya njema na nguvu zakutosha kutembea.

Leo niliswali swala ya Ijumaa katika msikiti uliopo karibu na eneo la College ninayo soma, ambapo Muhutubu (imam wa msikiti) alitoa hotuba iliyoenda na annuani ya mambo manne muhimu kwa kila muislamu.

Mambo hayo manne ni kutafuta elimu ya kumtambua Mola muumba, kuifanyikazi elimu uliyoipata katika matendo, kukataza mauvu na kuamrisha mema na la mwisho ni Subra.

KUTAFUTA ELIMU.

Kutafuta elimu ndio amri ya kwanza kupewa mtume Muhammad (s.a.w) pale alipo ambiwa asome akiwa katika pango la Hiraa. Amri ya kusoma inapatikana katika Quran sura ya 96 aya 1-5, hizi ndizo aya za mwanzo kushuka kwa Mtume (s.a.w).

Katika kuonyesha ubora wa elimu, Allah (s.w) anatuambia katika Qur an kuwa Adam (a.s) alimpatia elimu baada ya kumaliza kumuumba.

Elimu zote utakazo soma zikupelekee kwenye kumuogopa Allah (s.w). Elimu ya kumtambua Mola muumba ni yalazima kwa kila Muislam mwanamke ama mwanaume, na huku elimu za taaluma mbalimbali kama uwalimu, udaktari, uandisi, uhasibu, uwanasheria na nyinginezo, si lazima kwa kila muislam kuwa nazo lakini endapo katika jamii husika itamkosa mtu aliyebobea katika taalum hiyo, jamii zima itakuwa masuulia juu ya hilo.

KUFANYIA KAZI ULIYOYASOMA.

Mtu mwenye elimu lazima watofautiane na yule asiyekuwa na elimu katika ufanisi wake wa matendo. Mtume (s.a.w) anasema hawawezi kuwa sawa yule mwenye elimu na yule asiyekuwa naye.

Mwenye elimu atakuwa sawa na yule asiyekuwa nayo kwa kushindwa kuweka kwenye matendo ya kile unacho kisoma. Tutakuja ulizwa siku ya Qiyama tumeitumiaje elimu tuliyopewa na Allah (s.w).

Kama umesoma kumhofu Allah (s.w), lazima ujiepusha na mambo aliyo yakataza Allah (s.w) katika maisha yako ya kila siku ndipo hapo utasema nimeadhirika na elimu uliyoipata, na hiyo elimu itakuwa na manufaa kwako hapa duniani na Kesho akhera.

KUAMRISHA MEMA NA KUKATAZA MAOVU.

Kazi ya da'awa ni ya kila muislam katika nafasi yake kuifanya. Kazi ya kuondoa mauvi katika jamii ni ya kila mtu pamoja na kuamrisha mema.

Da'awa njema na iliyobora ni ile inayoanzia kwako mwenyewe kisha uelekee jamii kwa kuanza ndani kwako.

SUBRA.

Katika maisha ya kila siku kuna maudhi na mitihani ya kila namna ambapo ina itaji uvumilivu kuyashinda hayo yote.

Ukiingia katika kazi ya da'awa utakutana kila aina ya maudhi ya kulwamisha ama kukukatisha tamaa ya kutoendelea na da'awa, lakini uvumilivu na subra ndivyo hutakikana kati shughuli nzima ya da'awa.

Wabillah taufiq

0 comments