Friday, October 28, 2011

Chaneza yaigeuka Chaneta

CHAMA cha Netiboli Tanzania (CHANETA), kimesema wenzao wa Zanzibar (CHANEZA), wanawaweka njia panda kutokana na kushindwa kuthibitisha ushiriki wao katika mashindano ya Kombe la Uhuru yanayotarajiwa kutimua vumbi Novemba 30 hadi Desemba 8 kwenye viwanja vya Sigara, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Rose Mkisi, alisema toka walipotoa mwaliko wa kushiriki mashindano hayo, Chaneza haijawasilisha majina ya timu zitakazoshiriki.

Mkisi alisema kuwa walitoa mwaliko wa timu mbili kutoka visiwani humo ambapo walijaribu kuwasiliana nao kujua timu zitakazoshiriki, lakini walijibiwa kuwa hadi watakapofanya mkutano ndipo zitajulikana.

“Huo ni mwaliko ambao tumewapa wenzetu lakini tunaona wako kimya hawatujulishi kinachoendelea, hata hivyo hatupati shida sana, kwa sababu unapoalikwa ni hiyari yako kwenda au kutokwenda,” alisema Mkisi.

Kaimu Katibu Mkuu huyo, alisema, maandalizi yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na timu kujifua, ambazo ni JKT Mbweni, Filbert Bayi, Jeshi Stara, Magereza Morogoro, Hamambe, Polisi Mbeya, Polisi Dar es Salaam na Tamisemi Dodoma



Tanzania daima

0 comments