BONDIA Deo Njiku wa Morogoro amemchapa Anthony Segu wa Dar es Salaam katika mpambano wa kuwania ubingwa wa taifa wa Oganizesheni ya Ngumi Tanzania, TPBO, uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Katika mpambano huo, Njiku alimchapa Segu katika raundi ya 10 na bondia huyo alianza kumtwisha makonde tangu raundi ya kwanza na ilipofikia raundi ya 10 alisalimu amri.
Kocha wa Njiku, Boma Kilangi alisema kuwa mpambano huo ulikuwa mzuri licha ya kuchelewa kuanza. Hata hivyo, kabla ya mpambano huo, Seba Temba na Johanaá walitoka sare katika mapambano ya utangulizi huku Albert Mbena akimtwanga Kudra Taminu kwa pointi.
Mwananchi
0 comments