Wednesday, October 26, 2011

Safari lager kuidhamini timu ya Taifa ya pool

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imetangaza kuidhamini timu ya Taifa ya pool itakayoshiriki mashindano ya Afrika ya mchezo huo yatakayofanyika Blantyre, Malawi.

Mashindano hayo yajulikanayo kama All Afrika Cup 2011 Blantyre, Malawi yanatarajiwa kuanza Novemba 22 hadi Novemba 26 mwaka huu.

Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema bia yake imekuwa mdhamini mkuu wa
mchezo wa pool hapa nchini na imekuwa ikiidhamini timu hiyo tangu mwaka 2008 kwenye mashindano ya Afrika na Dunia.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Denis Lungu alitangaza majina ya wachezaji watakaoingia kambini kwa ajili ya mchezo huo ambao ni Omary Akida, Felix Atanas, Godfrey Mhando, Mohammed Iddy, Ally Akbar, Boniface John, Baraka Joakim, Jagory Makenzi, Antony Thomas, Ramadhan Ally, Emmanuel Loya, Shamis Nassor, Charles Venance, Abdallah Hussein na Emmanuel Sanka.

Naye Katibu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga alisema, katika mashindano ya mwaka huu ya yanatajiwa kushirikisha nchi 14 ambazo ni Tanzania, Malawi, Zimbabwe, Cameroon, Zambia, Uganda, Swaziland, Reunion FFB, Reunion Arabas, Nigeria, Msumbiji, Morocco na Lesotho.

Akitoa salamu za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho, Isaac Togocho alisema mchezo wa pool umekuwa si mchezo tena wa kupoteza muda bali ni mchezo kama mingine na unaelekea kuwa ajira rasmi kwa vijana wa Tanzania.




Habari leo

0 comments