Wednesday, November 2, 2011

BAKWATA: Eidil Haji november 6

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, BAKWATA limetangaza siku ya jumapili november 6 mwaka huu kuwa siku ya Eid El Haji na swala ya Eid kitaifa itaswaliwa katika msikiti wa Masjid Al Farouq saa 1.30 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari inasema kuwa jumapili ya november 6 ambayo ni sawa na dhulhija 10 mwaka 1432 itakuwa siku ya eidil hajj.

"Kwa mujibu wa Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Muhidini Mkoyongore, Swala ya Eid Kitaifa itaswaliwa katika Masjid Al Farouq iliyoko BAKWATA Makao Makuu, kuanzia saa 1.30 asubuhi ikifuatiwa na Baraza la Eid." ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

0 comments