Katika kuelekea miaka 50 ya uhuru blog yako ya Aboodmsuni Na Soka La Bongo linapenda kushirikiana nanyi katika kuunda wanakandanda waliopata kulitendea haki soka la bongo ndani ya miaka 50.
Tunapenda kushirikiana nanyi wadau wa soka la bongo katika kuteuwa kikosi cha Stars cha miaka 50, Kocha bora kutokea ndani ya ligi kuu ya Tanzania, Kocha bora aliyeiongoza Timu za Taifa pamoja na mchambuzi aliyeleta changamoto nyingi katika soka la bongo.
Blog yako itapokea majina ya makocha waliopata kukochi Taifa Stars unae muona anafaa kuwa kocha Bora wa miaka 50 ya uhuru, hivyo hivyo kwa makocha waliopita mpaka wa sasa katika ligi kuu ya Bongo ambaye unamuona anavaa.
Jina la kocha litakalojitokeza zaidi ndie atakuwa kocha bora aliyewahi kufundisha timu za Taifa, hivyo hivyo kwa yule aliyetamba katika ligi kuu ya Bongo.
Vilevile tunataka kupata mchambuzi bora wa miaka 50 katika soka la bongo, na jina la mchambuzi atakae tokea zaidi ndiye ataibuka kidedea.
Hivyo hivyo kwa wachezaji watakao tokea zaidi katika vikosi tutakavyopokea ndiye ataingia kwenye mkosi wa Stars wamiaka 50 ya uhuru.
Tutumia katika aboodmsuni@gmail.com ama aboodmsuni@yahoo.com ama aboodmsuni@hotmail.com.
Abdallah H.I Sulayman
Mmiliki wa Aboodmsuni



0 comments