Sunday, September 30, 2012

HUDUMA ZA AN KUREJEA OKTOBER 6


Baada ya kukosekana kwa huduma za Aboodmsuni Network katika mwishoni mwajuma lililopita na hili linalokwisha mda si mrefu, tunataraji kurejea katika mwisho mwajuma lijaro (oktobar 6 na 7).

Aboodmsuni Network inayotoa huduma ya ukarabati wa Computer, kubadilisha aina ya file (file converting) ambayo ipo chini ya uangalizi wa Mwanafunzi wa Diploma katika kitovu cha IT (Information Technology), Abdallah H.I Sulayman 'Aboodmsuni' itaendelea na utoaji wa huduma ya Ukarabati kwa sasa huku wakisitisha huduma ya File Converting kwa mda.

Huduma ya File Converting inasimama kutokana na kuharibika kwa kifaa kilichokuwa kinafanya kazi hiyo, hivyo basi huduma hiyo itarejeshwa pale kifaa hicho kitakapo kubali kufufuka kwa kununua kifaa kilicho ungua ndani ya mtambo huo, ama kuchukua mtambo mpya.

Kumbuka Aboodmsuni Network inafanya kazi siku za mapumziko kutokana na kuwa chini ya mtu mmoja anaekabiliwa na jukumu la kitabu katika siku za kawaida za kazi.

Kama unatatizo la Computer basi Aboodmsuni Network itakutatulia. Wasiliana Nasi kupitia 0787600613.


Imetolewa na: ABDALLAH H.I SULAYMAN 'Aboodmsuni'
Mmiliki na msimamizi pekee wa Aboodmsuni Network

No comments:

Post a Comment