Monday, September 10, 2012

LIGI KUU ZANZIBAR YAIREJESHA SIB

Ligi kuu ya Zanzibar inayo endelea kurindima katika viwanja mbalimbali visiwani Zanzibar vimepelekea kuto kufungwa kwa blog ya michezo inayomilikiwa na ABOODMSUNI NETWORK inayo kwenda kwa jina la SPORTS IN BONGO(SIB).

SIB ilikuwa ifungwe jumapili ya september 16 ikiwa ni siku moja baada ya ligi kuu ya Tanzania Bara kuanza kurindima kwa sababu ya msimamizi pekee wa blog hiyo Abdallah H.I Sulayman 'Aboodmsuni' kubanwa na kitabu pamoja na shughuli nyingine za ABOODMSUNI NETWORK.

Kutokana na hali hiyo ABOODMSUNI NETWORK iliona si ustaarabu kuiacha blog hewani wakati hakuna jipya linalo wekwa, na kama itawekwa taarifa mpya itakuwa ni ya kukopi toka katika blog nyingine.

Haipendezi kwa blog kuwa na asilimia 90 ya taarifa zako niza kukopi na hapo ndipo ilikuwa imefikia SIB ambapo ilitoka katika asilimia 70 mpaka 99 taarifa zake zilikuwa ni za kukopi.

Hivyo hatukuwa na budi zaidi ya kufikia uwamuzi wa kuifunga blog yetu hiyo ya michezo hapo september 16, lakini uwamuzi huo umevunjika baada ya kupata mwakilishi toka Zanzibar, ambaye atakuwa anatujuza kinachojiri ndani ya ligi kuu Zanzibar.

Kutokana na kupata mwakilishi huo tunaimani tutashuka kutoka 99% mpaka kwenye 70% ama chini yake katika suala zima ya kukopi toka katika blog nyingine, hivyo basi hatuoni haja ya kuifungia blog yetu zaidi ya kuwakaribisha wawakilishi wengine katika suala zima la kuiendesha SIB.

Katika urejeo wa SIB hakuto kuwa na kurasa ya WACHEZAJI, MAGAZETI bali kutaongezwa kurasa ya MITAA YA MICHEZO itakayo beba taarifa zinazo wekwa na mitandao mingine ya ndani na nnje ya nchi katika suala zima la michezo, NNJE YA MICHEZO itakayo beba taarifa na matukio nnje ya Michezo.

Hivyo basi ukiwa ndani ya SIB utaweza kusoma kilichopo katika mitandao mingine.

Ni matumaini yetu mutaufuraia urejeo wa SIB ukiwa na Mabadiliko hayo lakini kukipooza katika suala zima la utoaji wa Taarifa nnje ya ligi kuu ya Zanzibar na ucheleweshwaji wa taarifa za ligi kuu ya Tanzania Bara.


Imetolewa na ABDALLAH H.I SULAYMAN
Blogger wa SIB na Mmiliki wa Aboodmsuni Network

No comments:

Post a Comment