Thursday, September 27, 2012

MSUNI ATUNGULIWA NA MADOGO WA COSOVO

Aliyepata kuwa kipa namba moja wa Cosovo 'Eleven Boys' ya Morogoro, Abdallah Hamdun Sulayman 'Msuni' jioni ya leo ameingia kwenye nyavu na kuokota mipira mara 3 baada ya timu yake kukubali kufungwa goli 3.

Cosovo kwa sasa inaundwa na vijana wenye umri chini ya miaka 17 ambapo Msuni alikabidhiwa milingoti baada ya kuchelewa kwa kipa watimu hiyo, Said kukumbushia enzi zake.

Msuni ambaye timu yake iliundwa na vijana ambao wanaonekana wakubwa katika timu huku timu nyingine ikiundwa na wachezaji wengi wadogo na kufanikiwa kumtungua Msuni mara 3.

Katika mazoezi ya leo Msuni alikunwa na kiwango cha dogo anae kadiriwa kuwa na miaka 10 ambae alicheza kama beki wa kulia lakini kadri mchezo ulivyo kwenda ilimbidi acheze namba 4 ambapo aliimudu vyema nafasi hiyo na kuondoa hatari zote langoni mwake na kufanya maamuzi sahihi na ndani ya wakati.

Msuni kwa sasa makazi yake yako Dar es salaam na akiwa ameachana na Soka na kujikita katika shughuli za Aboodmsuni Network pamoja na kitabu.

Msuni alienda Morogoro alhamisi ya wiki jana kwa ajili ya kuweka mambo sawa katika harakati ya kutoka kwenye ukapera na huenda jumapili ya september 30 akarejea jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment