Tuesday, October 9, 2012

MSERBIA KUWANOA KINA DIDA AZAM

Mabingwa wa Mapinduzi na wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya kombe la shirikisho mwakani, Azam FC wameliongezea nguvu benchi lake la ufundi kwa kumuongeza Mserbia Sloboda.

Sloboda atakuwa na jukumu la kuwanoa makipa wa Azam FC wanaongozwa na Mwadini Ally, Deo Munish 'Dida' na Aishi Salum.

Msemaji wa Azam FC, Japhary Iddi Maganga amesema kuwa Mserbia huyo ni chaguo la kocha mkuu wa sasa wa Azam FC Boris Bunjak 'Boca' ambaye pia ni Mserbia.

Sloboda ataanza kazi na kuonekana katika benchi la Azam FC mara baada ya kupata kibali cha kazi

No comments:

Post a Comment