Tuesday, March 19, 2013

TAHADHARI KWA WATUMIAJI WA MITANDAO

Nikiwa nchini Sudani mwaka 2010 nilipokea barua pepe toka kwa mdada mmoja aliyekuwa anadai anataka kufanya ubia wa kibiashara na mie. Baada ya mawasiliano ya wiki kadhaa ya namna biashara itakavyo fanyika na fedha alizo nazo kama mtaji, nilitaka ushauri kwa dada zangu ambao walinitoa katika mtego huo.

Kuna ujumbe mwingi ambao hutumwa katika barua pepe zetu na watu wa mfano huo wakidaia ni watoto wa wakuu wa nchi ambazo kulitokea ama kuna machafuko ya kupigana wenyewe kwa wenyewe, mchezo ambao umewaliza wengi wenye tamaa ya hizo pesa wanazo tajwa.

Mchezo huo umezoeleka katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo huu wa facebook ambao unatazamwa kuwa na watumiaji wengi.

Kwenye facebook ambao kuna kila aina ya udanganyifu ambao huwapelekea watu kutapeliwa ila uliotawala katika siku za hivi karibuni, ambao watumiaji wengi wa facebook wamekuwa wakinaswa.

Kuna account zenye majina ya kike, sina uhakika kama account hizo zote zinaendeshwa na kinadada/kinamama kama taarifa zinavyo kuwa zikionyesha. Kazi kubwa wanayofanya ni kushawishi huhusiano ambao mwisho wa siku anaanza kukuomba umtumie pesa na pale unapo sisitiza kukutana nae huwa ndio mwisho wa mawasiliano.

Umakini unahitajika hususani katika hizi huduma za mitandaoni la sivyo utajikuta una nungunika pekee yako.


--
MSUNI COMPUTER SOLUTION
TUNATATUA TATIZO LA COMPUTER YAKO
065 718 4421
065 714 8283 (habib)
www.aboodmsuni21.blogspot.com

No comments:

Post a Comment