Msimu wa ligi kuu ya vodacom 2012/13 ulihitimishwa mei 18 kwa kushuhudia yanga wakitwaa ubingwa, ambao uliongezwa chachu kwa kufanikiwa kuchukuwa pointi 4 toka kwa mtani wake Simba sc baada ya kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo wa awali na mchezo wa pili kumfunga goli 2-0 katika ufungaji wa msimu.
ABOODMSUNI NETWORK inawapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi kwa ujumla kwa kuwezesha kuwapa furaha mashabiki na wanachama wa yanga sc.
Mmefanikiwa kuchukuwa ubingwa wa bara kitendo ambacho kimekuwa kawaida baada ya kuchukuwa ubingwa wa 24 mnaelekea kwenda kutetea ubingwa wa Afrika mashariki na kati, huku wadau wa soka tukitamani kushuhudia angalau mfikie katika hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika ambapo mnataraji kushiriki mwakani.
Mnatakiwa mjipange katika kuiwakilisha vyema nchi katika michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.
Vilevile tunachukuwa fursa hii kwa wafuatiliaji wa blogi za www.azamfans.blogspot.com na www.sportmsuni.blogspot.com watuwie radhi kwa kushindwa kufanya update katika kurasa za blog hizo katika msimu uliokwisha wa ligi.
Tulipata changamoto kuelekea mwishoni mwa mwaka jana na sasa taratibu tumeanza kuzishinda changamota na kuanza kurejea katika hali yetu ya kawaida, japo kuwa tuna enda kwa kasi ndogo.
Ni matumaini yetu kabla ya kuanza msimu ujao mambo yatakuwa sawa katika upande wa BLOG ZA MSUNI na kupelekea blog zetu kuwa na ubora uleule wa mwanzo ama zaidi ya pale.
Imetolewa na: ABDALLAH H.I SULAYMAN
Mmiliki wa ABOODMSUNI NETWORK.
No comments:
Post a Comment